VICHWA MBALIMBALI

NENO LA LEO



Yesu alipofufuka aliwaambia wanafunzi wake: “Tazameni mikono yangu… ya kuwa ni mimi mwenyewe. Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake…” (luka 24:39,40)
Jambo hili alilifanya ili kuthibitisha ya kuwa amefufuka na kwamba ni yeye Yesu Kristo wa Nazareti. Baada ya kusoma habari hii, yalinganishe na maneno haya: “Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika…mambo yote utakayotia mkono wako…katika nchi akupayo Bwana Mungu wako” (kumbukumbu 28:8).
Kwa kuyasoma maneno hayo ninataka ujue ya kuwa Damu ya Yesu ina uwezo wa kukusaidia kufanikisha kazi ya mikono yako! Hii inahusu uchumi wako na pia maisha yako, na jambo lolote unalotumia mikono yako kulifanya!
Kwa hiyo, ukiona unakwama katika maeneo hayo usisite kuomba Damu ya Yesu ikusaidie. Ikiwa umekosa hukufuata maagizo ya Mungu juu ya eneo hilo (kumbukumbu 28:1,2), usiache kutubu ili usamehewe na Damu ya Yesu ikupe kuanza upya! Na ikiwa ni shetani anakwamisha mafanikio ya kazi za mikono yako, uwe na uhakika ukiomba Damu ya Yesu ikusaidie basi utakwamuliwa!

No comments:

Post a Comment

Injili ya Yesu Kristo Designed by INNJILI TANZANIA Copyright © 2013-2015

Injili Tanzania Blog. Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.