VICHWA MBALIMBALI

DAMU YA YESU

Tunaposoma kitabu cha Luka 24:39,40 tunajua ya kuwa Yesu aliposulubiwa, mikono yake na miguu yake iliacha alama za kusulubiwa kwake. Hii ni dhahiri ya kuwa damu yake ilimwagika toka miguuni mwake, na toka mikononi mwake.
Damu ya Yesu Kristo kumwagika toka miguuni mwake ilikuwa ni ishara ya nini kwa wote wanaomwamini kama Bwana na Mwokozi wa maisha yao? Umwagikaji huu wa Damu toka kwenye miguu ya Yesu Kristo inakupa wewe:
1. Uhalali wa kumiliki eneo unalokanyaga kwa miguu yako! SomaYoshua 1:3, Kumbukumbu ya Torati 11:24.
2. Uhalali wa kuomba uongozi wake juu ya hatua za kukanyaga unapokuwa ndani yake! Soma Zaburi 37:23, 24, 31.
3. Uhalali wa kupeleka neno la Mungu kwa wengine ukiwa na uhakika wa msaada wa Mungu! Soma Warumi 10:15.
4. Uhalali wa kuomba Roho Mtakatifu akupe msaada wa kuenenda kwa imani! Soma 2Wakorintho 5:7
5. Uhalali wa kuwa na mamlaka ya kuzishinda nguvu za shetani. Soma Zaburi 91:13 na Luka 10:18, 19.


Mwl. C. Mwakasege

No comments:

Post a Comment

Injili ya Yesu Kristo Designed by INNJILI TANZANIA Copyright © 2013-2015

Injili Tanzania Blog. Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.