VICHWA MBALIMBALI

"UJUE ULIMWERNGU WA ROHO" na Mwl. Christopher Mwakasege

Ujue Ulimwengu wa roho.

Kitabu kipya kilichotoka mwezi huu wakati wa semina ya Dar es salaam.
Katika kitabu hiki utajifunza mambo mengi yanayohusu ulimwengu wa roho katika mpangilio wa sura kumi kama ifuatavyo;
1. Kufahamu umuhimu wa kujua uhalisi wa kuwepo kwa ulimwengu wa roho.
2. Kwa njia ya maombi unaweza kuwa mahali kiroho ambapo huwezi kuwa kimwili.
3. Mtu aliumbwa aishi katika maeneo mawili kwa wakati mmoja.
4. Mungu anakukaribisa katika ulimwengu wa roho ushiriki maamuzi pamoja naye kwa njia ya maombi yako.


  5. Kufanikiwa kwako katika maombi kunategemea unavyoitunza na unavyoitumia nafasi yako uliyonaayo katika ulimwengu wa roho.
6. Tambua umuhimu wa nafasi unayoitumia unapomwomba Mungu.
7. Chanzo cha mamlaka uliyonayo katika ulimwengu wa roho kwa njia ya maombi.
8. Umuhimu wa kujijua unajulikanaje katika ulimwengu wa Kiroho.
9. Inawezekana Mungu amejibu maombi yako ila yamekwama katika ulimwengu wa roho.
10. Kwa maombi yako ingia katika ulimwengu wa roho ili ubadili hali ya ulimwengu wa kimwili.
Unaweza kupata nakala yako katika ofisi zetu zilizopo Dar es salaam jengo la Luther house au Arusha mjini karibu na ofisi za tanesco. Pia kinapatikana katika semina zetu mbalimbali.

2 comments:

  1. Je? Unafahamu kuwa Mungu alishamtuma Eliya katika kizazi chetu, kama alivyoahidi katika Malaki 4:4-5, Naye ameshaleta ujumbe aliotumwa na kuondoka. Mungu alimtuma William Branham kama Eliya kutangaza ujio wa pili wa Kristo, ishara na miujiza iliyopita kiasi ambayo haikuwahi kutendeka hata sasa iliambatana na huduma yake, Fahamu sasa ujue ni wakati gani tunaishi na ni jinsi gani KRISTO yupo mlangoni kurudi.
    http://wingulamashahidiwakristo.blogspot.com/2016/09/mahojiana-ya-ndugu-william-branham_78.html#links

    ReplyDelete
  2. Asante kwa mafundisho mazuri naombi kwa mwalimu uviachie vitabu vyako kwa njia mtandao (online book) au (soft copies),ili nasi tujipatie vitabu hivi, asante

    ReplyDelete

Injili ya Yesu Kristo Designed by INNJILI TANZANIA Copyright © 2013-2015

Injili Tanzania Blog. Theme images by Jason Morrow. Powered by Blogger.